Tanzania jarida Octoba 2017

Rafiki Mpendwa,
Tunafuraha kupendekeza kwako toleo maalum la jarida linaloelezea kuhusu siku ya kimataifa ya kuushinda umaskini uliokithiri tarehe 17 mwezi wa 10. Kama unavyofahamu mwaka huu tutaadhimisha maadhimisho ya miaka 30 ya siku hii lakini si hivyo tu. Katika muundo wa wito wa kampeni ya kuchukua hatua, pia tutasherehekea maadhimisho ya miaka 100 ya Joseph Wresinski na miaka 60 ya shirika letu. Tukifuata muendelezo uleule wa mara ya kwanza.

Katika mwaka huu mzima sisi wanakamati wa Kamati ya Maandalizi ya Oktoba 17 tumekuwa tukiandaa tukio hili kulifanya kuwa fursa kwa watu wanaoishi katika umaskini uliokithiri waweze kusikika katika jamii. Tulitaka kuwashirikisha kwa upana wanachama wetu hai na kuwahakikishia ushiriki na uwepo wa kila mmoja. Maadhimisho ya pekee yanaratibiwa kwa ajili ya tarehe 14 mwezi Oktoba 2017 jijini Dar es Salaam.

Katika ukurasa wa 3 utaweza kusoma hutuba ya Joseph Wrisinski ya “ninatoa ushuhuda kwako” aliyoitoa tarehe 17 Oktoba mwaka 1957 katika uwanja wa Haki za binadamu jiji Parisi Ufaransa. Tukifuata moyo huo tumepanga utaratibu utakaounganisha sauti zetu na za wale wanaoishi katika ufukara, wakipambana kila siku kukabiliana na mazingira yao. Kama unavyofahamu mwaka huu Shirika la ATD Dunia ya Nne limeratibu kampeni inayoitwa UMASKINI BASI, iliyozinduliwa rasmi tarehe 12 Februari 2017. Kampeni hii inalenga kukusanya idadi ya watu wanaotaka kutokomeza umaskini uliokithiri duniani kote. hii ni namna ya kuonesha mshikamano wetu pamoja na watu wanaopigana dhidi ya umaskini uliokithiri.

Katika ukurasa wa mwisho tunakukaribisha kusoma tafakari za vijana, mustakabali wa jamii yetu. Ujumbe wa vijana wanne kutoka katika kikundi cha vijana ambao ni Agatha, Halfani, Pazi na Vicky ambao walikwenda Bukavu Congo kushiriki katika semina iliyohusu Elimu kwa Amani. Walishirikishana fursa walizokuwa nazo kugundua kujitolea kwao. Kama Vicky alivyosema, “ushirikiano kutoka katika makundi ya matabaka mbalimbali unaleta amani kwa sababu katika umoja tunaonekana kuwa wamoja.”’

Tunawatakia marafiki wote kila mahali Tanzania na kote duniani mafanikio na furaha katika siku ya Oktoba 17.

Sisi Kamati ya Maandalizi ya Oktoba 17. ATD Dunia ya Nne Tanzania TAHARIRI JARIDA LA OCTOBA 2017.

Kuendelea kusoma jarida hili, download PDF