Tanzania

ATD Tanzania inafanya kazi katika maeneo matatu ya Dar es Salaam: Soko la Samaki Magogoni, machimbo ya mawe karibu naTegeta, Boko na Tandale.

Timu yetu inafahamika sana  katika jamii hizo kwa sababu ya kujenga mahusiano nao ya muda mrefu, kwa kuzingatia uaminifu na ushirikiano wa kweli. Shughuli za pamoja kama vile madarasa ya elimu ya watu wazima, usajili wa vyeti vya kuzaliwa, kusaidia watoto kuhudhuria shule, kushirikiana ujuzi na wazazi vijana, akina mama na maktaba ya  mtaa na shughuli na  kundi la vijana. Kila mwaka upangwa tukio la kuadhimisha Oktoba 17, Siku ya Kimataifa ya kutokomeza umaskini.

ATD Dunia ya Nne imekuwa NGO iliyosajiliwa kufanya kazi katika Tanzania tangu mwaka 1999.

unaweza kupokea jarida letu kwa njia ya posta au barua pepe tafadhali wasiliana na.

Maelezo ya kuwasiliana