Sherehe za tarehe 17 Oktoba 2010 katika Tanzania

Siku ya kimataifa ya kupambana na umaskini uliokithiri duniani katika Tanzania ilisherehekewa Dar es Salaam katika ofisi mpya ya ATD Dunia ya Nne iliyoko Mwananyamala.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Changamoto kwa vijana katika mapambano ya kuushinda umaskini.

Watu zaidi ya 100 kutoka katika mashirika tofauti tofauti hapa Dar es Salaam na hata Njombe na Dodoma waliungana nasi na kushiriki katika tukio hili wakiwa na shuhuda, nyimbo na mashairi. Washiriki wengi walisisitiza juu ya umuhimu wa kupeana uzoefu hasa na wale walio maskini kabisa.

Pili ambaye anajihusisha na mradi wa kufuma kwa walemavu alituambia : “Tumejifunza kuwajibika kuwafundisha wale wanaojiunga na mradi kwa mara ya kwanza. Huu ni utamaduni wetu. Kila mtu anatakiwa kujihusisha na kutumia kipaji chake na kutoa kile alichojifunza mwanzoni alipojiunga na mradi.

Mariamu : Hutoa msaada sana kwa wafanyakazi wa soko la samaki ambao wanajifunza kusoma na kuandika “Pia mimi mwenyewe nilikuwa nikisaidiwa nilipokuwa na soma shule ya msingi. Naelewa umuhimu wa kusaidiwa. Najisikia fahari kuwa mmoja wa wasaidizi katika mradi huu wa kufuta ujinga. Vijana wamekuwapo mwaka huu pia :

  • Kwa upande mmoja, kikundi cha vijana marafiki wa ATD ambao walikuwa wakikutana katika kila Jumamosi ya pili ya mwezi, waliandaa shairi kuhusu umaskini na jamii na kumalizia kwa maneno haya:
    Tuungane kwa pamoja, tujeishinda kadhia,
    hala hala kila rika, penye nia pana njia,
    ufukara sio wimbo, kuuimba stejini,
    tuwekeze nguvu zetu, tuushinde umaskini.
  • Kwa upande mwingi, kikundi cha vijana marafiki kutoka Tandale waliandaa igizo lililoonyesha hatari na magumu wanayokumbana nayo katika maeneo yao kama : Umalaya, utumiaji wa madawa ya kulevya, kukosekana kwa heshima kati ya mdogo na mkubwa, uchafuzi wa mazingira na matatizo yake na mengine mengi.

Msanii ambaye ni mjumbe wa Uwaba ] (umma wa wapanda baiskeli) alimfanya kila mmoja kucheza na kupiga makofi kutokana na wimbo ambao unaweza kuuona kwenye kitembeza picha.

Play with Vimeo

By clicking on the video you accept that Vimeo drop its cookies on your browser.

October 17 Th 2010 in Tanzania from ATDFRA on Vimeo.