Tushirikiane kwa pamoja kama washiriki walio sawa

Kutokana na mradi ulioanzishwa Mei 2010, ATD Dunia ya Nne imekuwa ikisaidia familia zinazoishi katika umaskini uliokithiri kupata haki zao za msingi. Lengo la mradi huu ni kuonyesha kwamba umaskini uliokithiri unaweza kukabiliwa kwa ufanisi iwapo kutakuwa na ushirikiano kati ya watu waishio katika umaskini uliokithiri na wale ambao nyadhifa zao zinawapa mamlaka ya kuwa na uamuzi juu ya mahitaji ya watu ambao ni maskini kabisa (katika kuwaandikisha watoto shuleni, kutoa nakala za maombi fulani kwa watu hao n.k.).

Japokuwa ushirikiano huu unawezekana, bado si wa dhahiri. Kufanikisha ushirikiano huu, watendaji mbalimbali wanapaswa kufahamiana vizuri, kujua jinsi ya kufanya kazi pamoja na kuyatambua malengo shirikishi… Na huu ndio ujumbe wa warsha hii: “kufanya kazi pamoja kama washirika walio sawa”.