Tanzania Jarida September 2019

Ndugu wapendwa,
Ni matumaini yangu kuwa ni wazima wa afya na mnaendelea vizuri katika harakati za mapambano dhidi ya umaskini uliokithiri. Nasi hapa ATD Dunia ya  nne  tunaendelea  na  harakati  pamoja  na kuhakikiksha     shughuli     zote     zinaendelea tukianza  na  maadhimisho  ya  siku  ya  kutok- omeza  umaskini  uliokithiri  duniani  tarehe  17 Oktoba    2019  Kamati  ya  maandalizi    inaen- delea  na  maandalizi    ya  maadhimisho  hayo yatakayofanyika  katika  ukumbi   wa  chuo  cha ufundi stadi cha  Don Bosco kilichopo oyster- bay     ikisindikizwa   na   kauli   mbiu   isemayo “kushirikiana kwa pamoja kuwezesha watoto, familia   na   jumuiya   zao   katika   kutokomeza umaskini.”  Pia  tunaendelea  na  shughuli  za maktaba     ya     mtaa,     ambapo     inaendelea kuwezeshwa na vijana  wa ATD Dunia ya nne, katika  kuboresha  wawezeshaji  wamekuja  na wazo  la  kuwapeleka  watoto  maktaba  ya  taifa kwa ajili ya kujisomea. Hii inawafanya watoto kupenda      kusoma      vitabu      na      watoto wameipokea vizuri.

Baada  ya  kufanya  utatifiti  kwa  miaka  mitatu Kuanzia  mwaka  2016  hadi  2019,  mradi  huu wa    kubaini    vipimo    vya    umaskini    ume- hitimishwa   mwezi   juni   2019   kwa   kufanya kikao kikubwa na wadau mbalimbali  kwa ajili ya  mawasilisho  ya  vipimo  na  kuitambulisha mbinu    mpya    ya    utafiti    ya    kuunganisha maarifa    (MoK).    Pia    kwa    mwezi    uliopita kulikua  na  matukio  kadhaa  ikiwemo  semina ya  vijana   ililyofanyika  nchini  Rwanda   iliyo- husu mafunzo ya Tapori. Huu ni mtandao wa mawasiliano  wa  watoto  ambao  huwaleta  wa- toto   pamoja      na   kubadilishana   uzoefu   na maarifa ya watoto kutoka sehemu mbalimbali duniani kote. Pia kulikua na semina iliyohusu masuala ya fedha, semina hi ilihusisha wafan- yakazi  wawili  wa  kudumu  wa  ATD  Dunia  ya nne.   Mafunzo   hayo   yameweza   kuwajengea uwezo  mkubwa  katika  utunzaji  wa  fedha  na maadili yake.Vilevile vijana  wawili walikwen- da  kwenye  semina  huko  makao  makuu  Ufa- ransa. Semina hiyo ilihusu mawasiliano, kama tunavyojua mawasiliano ni kitu muhimu kati- ka  mwenendo  wetu  ili  kujua  taarifa  kutoka makao  makuu  na  kutoka  katika     maeneno mengine duniani kote.

Tumekuwa na upungufu wa wafanyakazi w kudumu wa ATD dunia ya nne hapa kwetu Tanzania baada ya wafanyakazi wawili ku- hamishiwa makao makuu Ufaransa, hili ni jambo la kawaida kiutendaji na lengo ni ku- kujifunza na kufanikisha shughuli za ATD Dunia ya nne.

Tunatumaini utafurahia kusoma jarida letu.
Venance F. Magombera

Kuendelea kusoma jarida hili, download PDF

0 comments Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.