Tanzania Jarida Aprili 2018

Hili ni jarida la kwanza kwa mwaka huu wa 2018. Tunayo furaha
kushirikishana nanyi habari tukitumaini kwamba mnaendelea vema mkiwa na nguvu katika majukumu yenu ya kila siku.

Kwa upande wetu tunaendelea vizuri. Tulikuwa na fursa ya kukaribisha watu mbalimbali ambao walijiunga na kusaidiana nasi
katika mambo kadhaa: Bwana Bruno Dabout mmoja kati ya timu ya uongozi wa kimataifa ya ATD, Bwana Martin Kalisa kutoka katika uongozi wa kanda ya Afrika, marafiki kutoka Kilimanjaro, Mbeya, Njombe, Dodoma na kadhalika….wote walishiriki pamoja nasi mnamo mwezi March katika tukio maalumu. Walishiriki kwa ukamilifu katika mikutano pia walikuwa msaada mkubwa katika kufaniksha jukumu letu.

Kwa ukamilfu kama ilivyokuwa imetaarifiwa katika jarida letu la mwishoni mwa mwaka 2017, tumehitimisha mradi wa Elimu kwa Wote kwa kuratibu semina ya kitaifa mwezi wa march 2018: Familia pamoja na watu mbalimbali tulikutana pamoja na kushirikisha namna walivyojitolea katika mradi. Washiriki walionesha hitimisho lao la jumla jinsi ilivyo muhimu kuwepo ushirikiano sawa katika kufikia mafanikio ya watoto shuleni. Tarehe 2 ya mwezi Juni, wafanyakazi wa kujitolea pamoja na marafiki watakuhudhuria katika semina ya kimataifa itakayofanyika Pierrelaye, makao makuu ya shirika ambapo shuhuda za elimu kwa wote zitatuwezesha kuelewa tulichojifunza kutokana na mafanikio ya mradi huu.

Utafiti wa vipimo vya umaskini unaendelea. Tumeanza kukutana na watu nje ya Dar-es-salaam katika mkoa wa Dodoma vijijini hususan katika wilaya za Kondoa na Bahi. Utafiti huu umetuonesha kwamba
hadi sasa haki za binadamu hasa kwa walio maskini bado zinakiukwa. Wakati mwingine mazingira duni hufanya hali kuwa mbaya zaidi. Kila mmoja wetu ameshuhudia majanga yaliyosababishwa na mvua kubwa mwezi uliopita ambapo idadi ya nyumba nyingi ziliathirika kwa mafuriko na baadhi ya watu kupoteza maisha na bado watu wengi wanataabika.

Tunatarajia kusonga mbele katika utafiti kwa kukutana na watu wa Njombe hivi karibuni. Haya ndiyo majukumu makubwa ambayo timu ilikuwa imelenga kuyatekeleza kipindi hiki. Tunawatakia heri wote. Wapeni moyo wale wote ambao wamepata athari kutokana na mvua hizi kubwa. Kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko.

Alexie Gasengayire, ATD Volunteer
Mwana katika Timu ya Uongozi.

Kuendelea kusoma jarida hili, download PDF