Tanzania Jarida September 2019
						Ndugu wapendwa,
Ni matumaini yangu kuwa ni wazima wa afya na mnaendelea vizuri katika harakati za mapambano dhidi ya umaskini uliokithiri. Nasi hapa ATD Dunia ya  nne  tunaendelea  na  harakati  pamoja  na kuhakikiksha     shughuli     zote     zinaendelea tukianza  na  maadhimisho  ya  siku  ya  kutok- omeza  umaskini  uliokithiri  duniani  tarehe  17 Oktoba    2019  Kamati  ya  maandalizi    inaen- delea  na  maandalizi    ya  maadhimisho  hayo yatakayofanyika  katika  ukumbi   wa  chuo  cha ufundi stadi cha  Don Bosco kilichopo oyster- bay     ikisindikizwa   na   kauli   mbiu   isemayo “kushirikiana kwa pamoja kuwezesha watoto, familia   na   jumuiya   zao   katika   kutokomeza umaskini.”  Pia  tunaendelea  na  shughuli  za maktaba     ya     mtaa,     ambapo     inaendelea kuwezeshwa na vijana  wa ATD Dunia ya nne, katika  kuboresha  wawezeshaji  wamekuja  na wazo  la  kuwapeleka  watoto  maktaba  ya  taifa kwa ajili ya kujisomea. Hii inawafanya watoto kupenda      kusoma      vitabu      na      watoto wameipokea vizuri.
Baada ya kufanya utatifiti kwa miaka mitatu Kuanzia mwaka 2016 hadi 2019, mradi huu wa kubaini vipimo vya umaskini ume- hitimishwa mwezi juni 2019 kwa kufanya kikao kikubwa na wadau mbalimbali kwa ajili ya mawasilisho ya vipimo na kuitambulisha mbinu mpya ya utafiti ya kuunganisha maarifa (MoK). Pia kwa mwezi uliopita kulikua na matukio kadhaa ikiwemo semina ya vijana ililyofanyika nchini Rwanda iliyo- husu mafunzo ya Tapori. Huu ni mtandao wa mawasiliano wa watoto ambao huwaleta wa- toto pamoja na kubadilishana uzoefu na maarifa ya watoto kutoka sehemu mbalimbali duniani kote. Pia kulikua na semina iliyohusu masuala ya fedha, semina hi ilihusisha wafan- yakazi wawili wa kudumu wa ATD Dunia ya nne. Mafunzo hayo yameweza kuwajengea uwezo mkubwa katika utunzaji wa fedha na maadili yake.Vilevile vijana wawili walikwen- da kwenye semina huko makao makuu Ufa- ransa. Semina hiyo ilihusu mawasiliano, kama tunavyojua mawasiliano ni kitu muhimu kati- ka mwenendo wetu ili kujua taarifa kutoka makao makuu na kutoka katika maeneno mengine duniani kote.
Tumekuwa na upungufu wa wafanyakazi w kudumu wa ATD dunia ya nne hapa kwetu Tanzania baada ya wafanyakazi wawili ku- hamishiwa makao makuu Ufaransa, hili ni jambo la kawaida kiutendaji na lengo ni ku- kujifunza na kufanikisha shughuli za ATD Dunia ya nne.
Tunatumaini utafurahia kusoma jarida letu.
Venance F. Magombera