Jarida la Juni 2012

Warsha ya ATD Dunia ya Nne, ’Tushirikiane Pamoja kama Washirika Walio Sawa’ iliyofanyika tarehe 20 na 21 Aprili 2012, iliwaleta pamoja watu wanaoishi kwenye umaskini uliokithiri na watu wanaofanya kazi kwenye nyanja za utawala (mf. mwalimu, daktari, afisa wa serikali za mtaa n.k.). Kupitia mradi wetu wa miaka miwili iliyopita, Upatikanaji wa Haki za msingi, tumeona kwamba mara nyingi kunaweza kutokea kutoaminiana na kuto-elewana baina ya pande hizi mbili…