Kushughulikia Vipimo Vilivyofichika vya Umaskini katika Maarifa na Sera

Tarehe 15 Februari 2024
Washington, D.C. na Mtandaoni

MAELEZO YA TUKIO

  • Tarehe: Alhamisi, Tarehe 15 Februari 2024
  • Saa: 9 am – 5 pm Majira ya ET

Hatua zilizopigwa katika kupunguza umaskini zimepimwa kimsingi kuhusiana na matumizi au mapato. Hata hivyo, vipengele vingine vya maisha ni muhimu sana kwa ustawi, na miradi kadhaa imekuwa ikitekelezwa ili kubuni vipimo vingi vya umaskini. Kongamano hili litawaleta pamoja wasomi, watoa huduma na watu wanaoishi kwa umaskini kama watafiti wenza ili kuelewa vizuri vipimo muhimu vya umaskini na uhusiano wake. Litaangazia pia zana ya Utathmini na Ufafanuzi Jumuishi wa Busara wa Sera (IDEEP, Inclusive and Deliberative Elaboration and Evaluation of Policies) ambayo imeundwa ili kubuni, kutekeleza na kutathmini vizuri sera, mafunzo au miradi, ambayo inalenga kushughulikia umaskini kwa kushiriki kikamilifu na kujumuishwa kwa watu wanaoishi kwa umaskini.

Kongamano hilo litatumia maarifa ya utafiti wa mradi shirikishi wa miaka mingi uliofanywa na shirika la International Movement ATD Fourth World, kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Oxford. Mbinu hii inachanganya maarifa kutoka kwa hatua zilizochukuliwa, utafiti wa kielimu na hali halisi za watu wanaoishi kwa umaskini, ili kutoa maarifa mapya kuhusu hali ya vipimo vingi vya umaskini na zana ya IDEEP ambayo inabadilisha matokeo ya utafiti huu kuwa vitendo. Wataalamu kutoka World Bank na IMF, pamoja na watafiti wa kielimu na watoa huduma, watatoa maoni na kuchangia mawazo yao binafsi. Washiriki wa kongamano watajadili jinsi ya kupiga hatua zaidi katika kupima umaskini, sera, mafunzo na kuchukua hatua.

MUHTASARI WA AJENDA

Saa 9:00 – 9:15 AM Hotuba za Ufunguzi

  • Donald Lee, Rais, International Movement ATD Fourth World
  • Antonio Spilimbergo, Naibu Mkurugenzi, Idara ya Utafiti, IMF
  • Luis Felipe Lopez-Calva, Mkurugenzi wa Kimataifa wa Umaskini na Usawa, World Bank

Saa 9:15 – 10:00 AM Hotuba Kuu: “Kutathmini Athari za Sera za Kupambana na Umaskini: Umuhimu wa Mbinu Nyingi”

  • Esther Duflo, Abdul Latif Jameel Profesa wa Upunguzaji wa Umaskini na Uchumi wa Maendeleo, Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts; Mshindi wa Tuzo ya Nobel katika Sayansi za Uchumi; Mwenyekiti wa Sera ya Umma na Umaskini katika Collège de France

Saa 10:00 – 11:15 AM The ATD Fourth World – Oxford University Vipimo Fiche vya Utafiti wa Umaskini

  • Wasilisho la jumla na watafiti wenza kutoka kwa Timu za Utafiti za Kimataifa na za Kitaifa

Saa 11:30 – 12:45 PM Warsha Sambamba kuhusu Kushughulikia Vipimo Fiche vya Utafiti wa Umaskini nchini Bolivia, Tanzania, Uingereza na Marekani (Ana kwa Ana Pekee)

Saa 1:30 – 2:30 PM Kuhusisha Watu Wanaoishi kwa Umaskini katika Utunzi, Utekelezaji na Utathmini wa Sera Zinazowaathiri: Uwasilishaji wa Zana ya Utathmini na Ufafanuzi Jumuishi wa Busara wa Sera (IDEEP, Inclusive, Deliberative Elaboration and Evaluation of Policies)

  • Olivier De Schutter, Katibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Umaskini Uliokithiri na Haki za Binadamu (UN Special Rapporteur on Extreme Poverty and Human Rights)
  • Xavier Godinot, Mkurugenzi wa Utafiti, ATD Fourth World

Saa 2:30 – 3:45 PM Warsha Sambamba kuhusu Kutekelezwa kwa Zana ya IDEEP nchini Bolivia, Tanzania, Uingereza na Marekani (Ana kwa Ana Pekee)

Saa 4:00 – 5:00 PM Mazungumzo ya Pamoja ya Kuhitimisha: Tunachukua Mwelekeo Gani?

  • Martin Kalisa, Naibu Mkurugenzi, International Movement ATD Fourth World
  • Ceyla Pazarbasioglu, Mkurugenzi, Idara ya Sera ya Mkakati na Ukaguzi (Strategy Policy and Review Department), IMF
  • Olivier De Schutter, Katibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Umaskini Uliokithiri na Haki za Binadamu (UN Special Rapporteur on Extreme Poverty and Human Rights)
  • Luis Felipe Lopez-Calva, Mkurugenzi wa Kimataifa wa Umaskini na Usawa, World Bank

YANAYOHUSIANA

Zana ya Utathmini na Ufafanuzi Jumuishi wa Busara wa Sera (IDEEP, Inclusive and Deliberative Elaboration & Evaluation of Policies)
Vipimo Fiche vya Umaskini – Utafiti Shirikishi wa Kimataifa
ATD Fourth World – Tuko pamoja kwa hadhi
Shirika la Fedha la Kimataifa (International Monetary Fund)
World Bank – Umaskini

0 comments Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *