Tanzania Jarida Januari 2019

Mpendwa Rafiki,
Tunayofuraha kubwa kuwapasha habari kuhusu maadhimisho ya Oktoba 17 ya mwaka huu hapa Tanzania na sehemu mbalimbali duniani. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Pamoja Tujenge Dunia yenye kuheshimu Haki za Binadamu na Utu wa kilamoja”.

Kulikuwa na kamati maalum ya kuandaa maadhimisho ya siku ya Kuutokomeza Umaskini Duniani, kamati ilikuwa na watu tofauti vijana, wazee na watu wazima. Tungependa tuwashirikishe jinsi maadhimisho ya mwaka huu yalivyo sherehekewa, wadau kotoka matabata tofauti tofauti kama vile mashirika, viongozi wa serikali za mitaa, manispaa, bima za afya, walimu na watu kutoka Rita pamoja na familia waliweza kushirikiana nasi.

Lengo lilikuwa ni kushirikishana kuhusu njia na jinsi wanavyopambana kila siku kuutokomeza umaskini uliokithiri na pia kushirikishana mawazo mapya kutoka kwa wadau tofauti tofauti ili kutusaidia kupiga hatua kwenda mbele na hiki ndicho wanachokitaka wana familia. Wadau waliweza pata fursa kusikia ni kwa jinsi gani watu wanaoishi katika umaskini uliokithi ni wanavyopambana kila siku kuutokomeza umaskini. Ni watu wenye ujasiri mkubwa katika kupambana na umaskini na kuutokomeza, pia tukiungana na kushirikiana kwa pamoja itatupa njia /nafasi ya kujifunza sisi kwa sisi na kufikia malengo ya kuutokomeza umaskini.

Hii ni siku ya wadau wanaoishi katika umaskini uliokithiri na marafiki zao kujieleza na kupaza sauti zao kwa pamoja ili zisikike duniani kote kwa kusoma shuhuda zinanoelezea maisha yao na juhudi wanazozifanya katika kupambana na umaskini na kwa pamoja kutafuta njia bora ya kutokomeza.

Kwenye kurasa inayofuta utapata kusoma shuhuda zao.

Asante.
Salma Moshi
ATD Fourth World Tanzania

Kuendelea kusoma jarida hili, download PDF