2015 kwa changamoto mpya ya mafanikio ya elimu kwa wote!

Shule inatakiwa kuwa ni sehemu ya furaha, ambapo watoto wanaweza kujifunza, kujenga urafiki na kuboresha mahusiano ya kijamii. Watoto wataanza kujua maeneo yao na katika jamii zao na taratibu za kijamii. Wataongeza uwezo wa kufikiri kwa kina, kuuliza maswali na kugundua maajabu na miujiza ya dunia. Kukiwa na usawa wa elimu ni sawa kuipa uhuru jamii na kuwaondosha katika utumwa wa fikra.