Jarida la Februari 2013

« Lengo la ATD ni kuvunja tofauti zilizopo kati ya matajiri na maskini. Maskini wengi kama sisi wanadhani kuwa dunia ni ya matajiri na kwamba dunia hii siyo ya kwetu. La, siyo hivyo, dunia hii ni yetu wote. Maskini wengi hudhania kuwa, “Sisi maskini siyo watu muhimu na hatuna thamani. Tunaamini kuwa shule na hospitali ni kwa ajili ya matajiri, kama ilivyo kwa vitu vyote muhimu. Shuleni tunaona watoto wa matajiri wanasoma kupata elimu bora wakati ambapo watoto wetu wanadharaulika, na hata hospitali tunatengwa”… »