Kujenga maisha kwa sasa

Uchoraji: 2009, Hakimiliki – Kituo cha Joseph Wresinski AR0200703002 © Nelly Schenker

Ujumbe wa wana ATD Dunia ya Nne wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Kwa wakati huu ambao kila mtu anaishi  kwa mwendo wa polepole, bila uhakika wa maisha, ambapo shida na mateso ya watu dhaifu zaidi vinaongezeka na vinakuwa na uzito mwingi, tunataka kurudia hamu yetu ya kukaa karibu pamoja kwa wengine na hasa katika hali ya pekee pamoja na hawa watu maskini zaidi, ili kukabili gonjwa hili pamoja. Tunaamini kuwa kushiriki juhudi za wote wanaotafuta kutomsahau mtu ni njia ya kutiana moyo.

Serikali ya Kongo imechukua hatua za kulinda idadi ya watu kwa kuhofia kuenea kwa ugonjwa huo haraka. Hivi sasa, uhamasishaji juu ya hatua za kuzuia hufanyika ndani ya miji bila kufikia maeneo ya pembeni ambapo kila kitu kinakosekana: barabara, madaraja, vituo vya afya, umeme na mahali ambapo mmomonyoko wa ardhi unatishia nyumba. Tunazikumbuka sana familia ambazo zinaishi huko katika ukosefu wa habari za uhakika.

Mara moja tuliunda timu ndogo nyingi ili kwenda maeneo ya mbali zaidi na kutembelea familia zilizotengwa zaidi. Kwa kweli, tumeelewa kauli mbiu: “Kinga wengine kwa kujilinda” na hiyo inamaanisha kufuata melekezo ya kujilinda yanayofuatwa ulimwenguni kote na kufahamu kuhusu virusi. Kwa hivyo tulianza kwa kujifunza kuhusu virusi na namna vinavyoambukizwa, nini cha kufanya ikiwa tunajisikia kuathiriwa na tunatoa mafunzo katika uhamasishaji.

.Sasa tunakutana na familia zisizoweza kufikiwa na habari ili kushirikishana maarifa haya kwa pamoja na kutafakari maana yake kwao na jamii zao. Pia ni wakati wa kufikiria juu ya familia ambazo hatuna habari nazo na kujaribu kuwasiliana nazo. Kwa hivyo tuliamua kwenda mbali iwezekanavyo na kupanda milima ya Cikera na Mushekere licha ya matope msimu huu ili kufikia familia zingine.

Watu ambao tunakutana nao wanapendezwa sana na wanatuambia waziwazi shida waliyonayo katika kujilinda. Familia hizi hazina uwezo wa kupata bidhaa za kujikinga na nyumba zao, lakini pia wanapata shida ya kupata maji safi. Jerikani moja ya maji iliyokuwa inagharimu kati ya faranga 50 hadi 100 za Kongo, leo inagharimu faranga 200 au zaidi. Hii ni moja ya udhalilishaji dhidi ya wale wasioweza kujitetea wakati serikali imeshaondoa bili za maji kwa familia zilizo maskini zaidi. Hatua hii haiwafikii walio maskini zaidi.

Tunahamasisha kwa kuongea na viongozi wa vitongoji ili wachukue hatua kwa wasambazaji wa maji kwa kukomesha vitendo hivi ili maji yapatikane kwa watu wote katika kipindi ambacho yanahitajika kwa ajili ya kulinda maisha. Kuna upungufu mwingi wa sabuni katika vitongoji, ila sisi tunazileta na kuzigawa kwa familia ambazo zinaishi katika mazingira magumu zaidi.

Tunaenda nyumba kwa nyumba kuzungumza na watu, wajisikie kwamba tuko pamoja katika kipindi hiki na kujifunza pamoja kile tunachoweza kufanya katika muktadha huu usiosemeka.

2020, DRC, Bukavu, Watoto wa jamii moja, wamefungwa kwa pamoja © ATD Dunia ya Nne

Katika ziara zetu, sisi pia tunachukua wakati na watoto. Wengi wao ni washiriki wa Tapori, ni wakati tunapojifurahisha ndio tunapata nguvu ya kufanya pamoja mazoezi ya vizuizi chini ya macho ya wazazi wao. Tangu mwanzo wa mwezi wa Machi, shule zimefungwa. Watoto lazima wabaki kwenye eneo lao. Wanasaidiana kwa kuchota maji na kuni pamoja, pia wanacheza kwa kujenga mfamo wa vijiji vidogo kwa kutumia mchanga. Hivi ndivyo wanavyoishi katika “kizuizi cha pamoja”.

Tunaendelea kueneza habari za Tapori kwa sababu tunajua jinsi ilivyo muhimu kwa watoto kuunganishwa na watu wengine. Mama mmoja alituambia kwamba Tapori ni bahati kwa watoto, inawahimiza wafikie matamanio yao kadiri ya ndoto zao.
. Tunaendelea pia kuwasiliana kwa simu na vikundi vinavyohusika katika sehemu zingine za nchi, huko Goma, Uvira na Kavumu, kwa kutiana moyo. Wao pia wanatafuta kuunganisha mshikamano na udugu uliobaki, zaidi ya kufuata maagizo ya kujikinga, silaha bora zaidi katika mapigano haya.

Kwetu sisi, ziara hizi na mahusiano haya vinatuambia tena zaidi maana ya kujitolea kwetu. Kama Rosine anasema: “Sisi, tunaishi na familia sio kampeni ya uhamasishaji dhidi ya virusi hivi, lakini ni uimarisho wa uhusiano na wazazi pamoja na watoto kwa sababu tunajisikia kuwa washiriki wa familia moja.” Naye Emmanuel anaongeza:

“Harakati zetu sio za kiutawala, tunaunda maisha pamoja, familia ambayo inamtambua kila mtu.”

 

0 comments Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *