Tanzania jarida Desemba 2017

Jarida hili ni hitimisho la mwaka mzima kwa harakati za ATD Dunia
ya Nne. Miradi iliyowakutanisha watu, kutambua mapambano katika maisha yao ya kila siku, kwa watoto wao, familia zao. Maisha yao yanatukumbusha tena kwamba tunajukumu la kufahamu na kuwafanya watu kutambua nini maana ya kuishi kwa kuto tambuliwa na kuheshimiwa.

Utafiti wa kubaini viashiria vya umaskini bado unaendelea vizuri. Timu inafanya kazi na wawakilishi wa makundi katika jamii ya Dar es Salaam. Wanaume, wanawake, watoto, wazee, walemavu, wagonga mawe, wanataaluma n.k.

Tutashirikishana mambo tuliojifunza, mikutano, shuhuda zinatualika kwa pamoja kutafakari upya nini maana ya kuishi katika umaskini uliokithiri, umaskini uliokithiri sio tu kukosa pesa. Ni ukosefu wa amani, usalama wa kudumu. Mama mmoja mpishi katika soko la samaki ambae huibiwa vitu alivyonavyo wakati wowote ule au mama mwingine ambae anagonga mawe hana jinsi na humchukua mwane
mdogo na kwenda nae machimbo ya kokoto na kumsaidia kazi. Mwaka 2018 tutakutana na watu wanaoishi kijijini.

Jarida hili pia ni maalum. Ni hitimisho la mradi wa Elimu Kwa Wote. Timu imeaandaa taarifa kutueleza taarifa tofauti kutoka katika mradi huu na kipi kilichofanikiwa. Mwaka huu 2017, mikutano ilivyoongeza uelewa na umoja baina ya walimu na wazazi kama ni njia moja ya mafanikio ambayo itawafanya watoto kuanza na kumaliza elimu yao ya msingi na kufikia malengo yao.

Pia tungependa kushirikishana nanyi katika siku muhimu ya mwaka, kwa kila mwaka, siku ya kutokomeza umaskini. Mamia ya wanaharakati hujumuika pamoja na kusema ni jukumu letu kuwa pamoja na wale wote wanaoishi katika hali ngumu na kufikia haki zao za msingi.

Nawatakia kheri ya mwaka mpya 2018 na nguvu na afya njema kwa kila mmoja kufikia melengo yetu ya kupambana na changamoto wanazokutana nazo watu wanaoishi katika umaskini.

Alexie Gasengayire
Mjumbe wa Timu ya Uongozi ya ATD

Kuendelea kusoma jarida hili, download PDF