ATD DUNIA YA NNE TANZANIA JARIDA Disemba 2015

Newsletter-2015-12-KISWA-B.pdf

Rafiki wapendwa,
Tunafurahi kuwashirikisha habari za hivi karibuni kutoka katika harakati zetu za ATD Tanzania katika miezi hii ya mwisho. Kipindi hiki kilikuwa tajiri katika mikutano na shuhuda, juu ya tukio la Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Umasikini Uliokithiri, siku ilisherehekewa katika maeneo matatu tofauti nchi: Njombe, Dodoma na Dar es Salaam. Maelfu na maelfu ya watu duniani kote kwa mara nyingine tena walionyesha umoja wao na dhamira ya dunia bila umasikini na heshima ya haki za kila mtu (tazama ukurasa wa mwisho
“Sherehe katika Afrika ya Kati”).

ATD Tanzania inajihusisha katika utafiti wa familia na shule kwa elimu kwa wote, hivyo tumechagua kusherehekea siku hii tukihusisha
na mada hii.

Elimu kwa wote bado ni changamoto kubwa kwa familia zinazoishi katika hali halisi, lakini pia ni changamoto kwa jamii nzima kwa sababu maendeleo ya jamii hayawezi kukamilika kama sehemu ya wakazi haina upatikanaji wa elimu.

Hata hivyo, jitihada zimefanyika kama mfano wa kuigwa. Mfano ni Njombe, Umoja wa wafua vyuma wa Kisangani ambapo kituo cha vijana kinatoa mafunzo ya kitaaluma ambayo yatawawezesha vijana kurejesha matumaini na kuwa na uwezo wa kuvunja mzunguko wa
umasikini kwa kupata maarifa na kazi. Pia inajenga mshikamano kati ya wale waliomaliza mafunzo yao na wale ambao wanataka kuanza
kujifunza.

Tunatumaini mnafurahia habari za hivi karibuni na tunapenda kuchukua fursa hii kuwatakia Heri kwa Mwaka Mpya wenye mafanikio uliojazwa na kujitoa kikamilifu katika jamii.

Katika urafiki,
Alexie Gassengayire
Mjumbe wa Timu ya Uongozi ya ATD