Upatikanaji Wa Msingi Ya Elimu Kwa Watoto Wanaoishi Katika Umaskini Uliokithiri – ATD Tanzania

“Elimu hunisaidia kufikia malengo ya ngu. Elimu ni ukombozi kwa maisha yangu, familia yangu na kwa jamii yangu”.

A primary school child, Kinondoni

Muhtasari wa Utafiti

Historia
Elimu ya msingi ni moja kati ya misingi mikuu katika maisha. Haki ya elimu ya msingi kwa mtoto siyo suala la mjadala, licha ya upana wa uchumi wa familia ya mtoto, utamaduni au asili ya jamii yake. Hata hivyo, kuhusu watoto ambao wanaishi katika familia ambazo zimezama katika ufukara mkuu uwezekano wa kumaliza mzunguko wa kumaliza elimu ya shule ya msingi unakuwa finyu mno. Utafiti huu shirikishi ulianza tangu Januari 2015 hadi Marchi 2016 katika wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam, kuelewa hali sahihi za watoto wanaoishi katika umaskini, kuanza na kumalizia masomo yao katika shule za msingi.

Mbinu
Watu wanaoishi katika umaskini uliokithiri wanao ufahamu unaotokana na uzoefu wao adimu wa maisha yao. Mara zote hawatazamwi na waishia kudharauliwa, ufahamu wao wa ndani unaweza kuleta utatuzi muhimu kwa changamoto wanapokaa meza moja na watunga sera. Utafiti ulihamasishwa, kuendelezwa na
kusaidiwa na timu iliyohusisha watu wanaoishi katika ufukara uliokithiri na wengine kutoka katika nyanja mbali mbali. Kwa zaidi ya miezi kumi na mitano walihojiwa wazazi arobaini na sita, watoto arobaini walimu ishirini na viongozi wa serikali za mitaa. Njia iliyo bora na sahihi ilitumika kuweza kupata ufahamu mpana kuhusu
familia zinazoishi katika ufukara uliokithiri. Katika mbinu hii timu ya utafiti iliweza kufahamu afya ya familia, pato, mahusiano mapana ya kijamii n.k. Yanavyokuwa na athari katika elimu ya msingi ya mtoto na kuibua juhudi zinazofanywa na wadau mbali mbali wanaohusika. Timu ya utafiti ilikuwa bunifu katika jinsi yake ya kukusanya na kuchambua takwimu kuhakikisha kila mtu licha ya asili yake
anachangia katika thamani iliyo sawa.
Mbinu hii wakati hali sahihi iliporuhusu ilionesha maoni ya watu wanaoishi katika ufukara uliokithiri kuwa yanaweza kutumiwa katika kutengeneza mabadiliko ya sera  ambazo zitaleta msukumo chanya katika jamii zao.

Matokeo
Elimu ya msingi kwa watoto wanaotoka katika familia zenye ufukara uliokithiri kwa mapana imejikita kwa sehemu mkubwa katika muktadha wa familia changanua, na jamii pana, migongano ya ndani na ya nje katika familia na jumuiya, afya na kazi za wazazi usalama na masuala mbalimbali yanayowazunguka na mazingira yote yanayosababisha athari kubwa kwa watoto. Kwa changamoto ambazo zinakuja mara kwa mara na bila kutegemewa, familia zinazoishi katika umaskini uliokithiri hutafuta ufumbuzi wake kadiri zinavyojitokeza nazo zinaweza kuwa za muda mfupi na zisizoeleweka. Mahusiano kati ya wazazi na walimu yanabadilika, ni ya kulaumiana na kuhukumiana. Watoto wanaogopa baadhi ya walimu wao na hujihisi kutengwa kutokana na asili yao. Yote haya huleta mzingira yenye changamoto kubwa kati ya watoto na walimu.
Hata hivyo nia ya kweli ya kuboresha mahusiano haya ilionyeshwa na wadau.
Juhudi zinafanywa, zingine ziko wazi wakati zingine zinahitaji uelewa. Elimu haina umuhimu ambao ni wa lazima kwa watu wanaoishi katika ufukara uliokithiri. Katika changamoto hizi mwalimu anabaki kuwa mtu aliyejitoa kuhakikisha anaelimisha.
Watoto kutoka katika familia zilizo katika ufukara uliokithiri huona kwamba elimu ni njia pekee ya kuwatoa katika dhima na tabu zao.

Mapendekezo
Mapendekezo yanaita ushirikiano kati ya washirika mbali mbali wanaofanya kazi katika kujitoa kuhakikisha kwamba mtoto anafanikiwa kuanza na kumaliza elimu yake ya shule ya msingi. Wazazi, walimu, viongozi wa serikali za mitaa na serikali kuu pamoja na jamii katika upana wake washirika wa nje pamoja na watoto wenyewe kila mmoja analo jukumu la kufanya katika utekelezaji wa hili.

Download.