ATD Tanzania inafanya kazi katika maeneo matatu ya Dar es Salaam: Soko la Samaki Magogoni, machimbo ya mawe karibu naTegeta, Boko na Tandale.
Timu yetu inafahamika sana katika jamii hizo kwa sababu ya kujenga mahusiano nao ya muda mrefu, kwa kuzingatia uaminifu na ushirikiano wa kweli. Shughuli za pamoja kama vile madarasa ya elimu ya watu wazima, usajili wa vyeti vya kuzaliwa, kusaidia watoto kuhudhuria shule, kushirikiana ujuzi na wazazi vijana, akina mama na maktaba ya mtaa na shughuli na kundi la vijana. Kila mwaka upangwa tukio la kuadhimisha Oktoba 17, Siku ya Kimataifa ya kutokomeza umaskini.
ATD Dunia ya Nne imekuwa NGO iliyosajiliwa kufanya kazi katika Tanzania tangu mwaka 1999.
unaweza kupokea jarida letu kwa njia ya posta au barua pepe tafadhali wasiliana na.
Maelezo ya kuwasiliana
Kushughulikia Vipimo Vilivyofichika vya Umaskini katika Maarifa na Sera
Tarehe 15 Februari 2024 Washington, D.C. na Mtandaoni MAELEZO YA TUKIO Tarehe: Alhamisi, Tarehe 15 Februari 2024 Saa: 9 am (…) Read more
MPAKA DENI LITAKAPOLIPWA
Picha © Guillermo DIAZ/AR0201602040 Baada ya kupitia changamoto nyingi, kwa pamoja Sophia mwanaharakati wa ATD kutoka maeneo ya Boko Dar (…) Read more
HATIMA GANI YA BAADAYE NINAYOHITAJI KWA MAKTABA YANGU YA MTAA?
Programu ya Maktaba ya Mtaa Tandale ni shughuli kongwe kuliko shughuli zote za ATD Dunia ya Nne Tanzania. Ilianza miaka (…) Read more